Jumatano 1 Oktoba 2025 - 07:04
Msaada wa Kina wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Nikaragua kwa Taifa Lenye Kudhulumiwa la Palestina

Hawza / Waziri wa mambo ya nje wa Nikaragua amevitaja vikwazo na hatua za upande mmoja za Marekani dhidi ya Cuba na Venezuela kuwa ni “uhalifu dhidi ya ubinadamu” na akatangaza kuunga mkono mapambano ya taifa lenye kudhulumiwa la Palestina dhidi ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Denis Moncada, waziri wa mambo ya nje wa Nikaragua, katika hotuba yake kwenye kikao cha ngazi ya juu cha mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, alikosoa kuendelezwa uvamizi wa kibeberu dhidi ya mataifa ya Amerika ya Kusini na dunia ya tatu. Alivitaja vikwazo vya kiuchumi, mzingiro na hatua za kulazimishwa upande mmoja dhidi ya Cuba na Venezuela kuwa ni “uhalifu dhidi ya ubinadamu” vinavyohatarisha usalama, amani na ustawi wa mataifa.

Moncada, kwa kurejelea “undugu wa kimapinduzi katika taifa kubwa” na urithi wa pamoja wa mapambano ya kupigania uhuru katika bara hilo, alisema: “Kama watoto wa mashujaa wa Amerika ya Kusini na washindi wa mapinduzi, tunatangaza mshikamano wetu kamili na usio na sharti na Cuba na Venezuela.”

Aidha alilaani kile alichokiita “mashtaka na upotoshaji usio na maana kuhusu suala la usafirishaji wa mihadarati”, na akasisitiza kuwa janga hili linajengeka katika nchi tajiri na vituo vikuu vya matumizi, ilhali nchi maskini zinakuwa wahanga wa uzalishaji wa kulazimishwa. Alionya: “Maumivu na mateso ya kibinadamu yamegeuzwa kuwa biashara na nyenzo za utawala.”

Waziri wa mambo ya nje wa Nikaragua alikataa kutumia visingizio hivi kwa ajili ya kuhalalisha kuingilia kati, vitisho vya uvamizi na ubeberu, na akavieleza kuwa ni sababu ya kudhoofika kwa amani ya dunia. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, huku akilaani “mauaji ya kimbari na ukatili wa kinyama wa utawala wa Kizayuni dhidi ya taifa lenye kudhulumiwa la Palestina”, alitangaza: “Tunaulaani utawala wa Kizayuni na nguvu za kikoloni, kibeberu na kifashisti zinazounga mkono.”

Moncada pia aligusia matumizi mabaya ya njaa, utapiamlo na kutelekezwa kwa familia, wanawake, watoto na wazee kama nyenzo za utawala, na akasema kuwa ni “aina mpya ya ukandamizaji na maangamizi ya pamoja”.

Mwisho, kwa kusisitiza misimamo ya kimapinduzi ya nchi yake, alisema: “Nikaragua na mapinduzi ya wananchi wa Sandinista, tunajiona kuwa wamoja na mapambano yote ya uhuru, kujitegemea na heshima ya mataifa ya dunia. Tunajua kwamba hatujiuzi na katu hatutasalimu amri.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha